Posts

Showing posts from April, 2019

Matokeo ya mechi za robo fainali UEFA Ueropa league leo April 11

Image
Michezo mbalimbali iliendelea jana viwanjani, ambapo arsenal alikuwa akichuana vikali dhidi ya napoli na kumpiga kipigo kikali cha mabao 2-0, huku chelsea nae akipata bao moja dhidi ya Slavia praha, villarreal achezea kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya valencia huku Benfica akimtandika mabao 4-2 Frankfurt

Tanzia: Msanii Jessie ambaye alikuwa zao la THT afariki dunia

Image
Aliyekuwa msanii wa Bongo Fleva kutoka THT, Jessie, amefariki dunia. Jessie ni dada wa msanii, Jolie. Mmoja kati ya wasanii kutoka THT, Mwasiti Almas ambaye amesema ni kweli kuwa msanii huyo amefariki dunia. “THT imepoteza jembe leo Ooh Jessie mdogo wangu,umeenda na wewe…ALLAH akupumzishe salama 😭😭😭😭😭😭,” aliandika Mwasiti kupitia Instagram yake. Hata hivyo Mwasiti hakuelezea chanzo cha kifo chake kutokana na kutokuwa sehemu rafiki kwaajili ya mazungumzo na kuahidi kuwa ataeleza taarifa zaidi. Marehemu Jessie enzi za uhai wake amewahi kufanya kazi kadhaa ikiwemo nyimbo ya ‘Mapenzi Kamali’ aliyomshirikisha Madee. Kwa mujibu wa taarifa za awali, kifo chake kimetokea hospitali wakati wa kujifungua Related Articles

Young Killer ft Walid – Nahisi

Image
Msanii wa muziki, Young Killer Msodoki ameachia video ya wimbo wake mpya uitwo, Nahisi akiwa amemshirikisha Walid. Video ya wimbo huo imeandaliwa na Holland and Zanzibar na Director Musa Msafiri wa Kwetu Studios.