Posts

Matokeo ya mechi za robo fainali UEFA Ueropa league leo April 11

Image
Michezo mbalimbali iliendelea jana viwanjani, ambapo arsenal alikuwa akichuana vikali dhidi ya napoli na kumpiga kipigo kikali cha mabao 2-0, huku chelsea nae akipata bao moja dhidi ya Slavia praha, villarreal achezea kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya valencia huku Benfica akimtandika mabao 4-2 Frankfurt

Tanzia: Msanii Jessie ambaye alikuwa zao la THT afariki dunia

Image
Aliyekuwa msanii wa Bongo Fleva kutoka THT, Jessie, amefariki dunia. Jessie ni dada wa msanii, Jolie. Mmoja kati ya wasanii kutoka THT, Mwasiti Almas ambaye amesema ni kweli kuwa msanii huyo amefariki dunia. “THT imepoteza jembe leo Ooh Jessie mdogo wangu,umeenda na wewe…ALLAH akupumzishe salama 😭😭😭😭😭😭,” aliandika Mwasiti kupitia Instagram yake. Hata hivyo Mwasiti hakuelezea chanzo cha kifo chake kutokana na kutokuwa sehemu rafiki kwaajili ya mazungumzo na kuahidi kuwa ataeleza taarifa zaidi. Marehemu Jessie enzi za uhai wake amewahi kufanya kazi kadhaa ikiwemo nyimbo ya ‘Mapenzi Kamali’ aliyomshirikisha Madee. Kwa mujibu wa taarifa za awali, kifo chake kimetokea hospitali wakati wa kujifungua Related Articles

Young Killer ft Walid – Nahisi

Image
Msanii wa muziki, Young Killer Msodoki ameachia video ya wimbo wake mpya uitwo, Nahisi akiwa amemshirikisha Walid. Video ya wimbo huo imeandaliwa na Holland and Zanzibar na Director Musa Msafiri wa Kwetu Studios.

Ruge aagwa leo jijini daresalaam

Image
Maelfu ya watanzania, waomboleza, viongozi wa nchi pamoja na wasanii nchini wameunga na kwa pamoja na familia ya Ruge asubuh ya leo katika kumuaga marehemu huyo aliyekuwa mkurugenzi wa clouds katika viwanja vya Karimjee jijini Daresalaam. Baada ya kuagwa mwili wa Marehemu utaelekea Mwl. J.k Nyerere Airport kwaajili ya safari ya kuelekea  Bukoba nyumbani kwao na marehemu ambapo kutakuwa na nyumba yake atakayopumzika milele.

Diamond platnumz awa gumzo juu ya kifo cha ruge

Image
Kufuatia kifo cha mkurugenzi mkuu wa clouds media group (CMG) Ndg.Ruge mutahaba, maelfu ya watanzania na wana burudani wakaa mkao wa kula wakisubir kuona nin msanii diamond platnumz atakachopost juu ya kifo cha Ruge, ambapo mpaka sasa msanii huyo hakuna alichoposti kwenye kurasa zake zote kuhusiana na kifo cha ruge.